Kufukuliwa kwa miili ya watu walioaminika kuzikwa kwenye kaburi la pamoja katika eneo la Ozi kaunti ya Tana river sasa kunatarajiwa kufanyika hapo kesho, mbele ya mpasuaji maiti mkuu wa serikali. Inspekta Mkuu wa idara ya upepelezi David Cheruiyot alifanikiwa kupata agizo la mahakama kufukua miili hiyo kwa uchunguzi kamili kubaini kilichosababisha vifo vya watu hao pamoja na maiti hizo kutambuliwa na familia na watu wa ukoo.
Read 645 Times|
Published in















