Saturday, 28 July 2012 17:59
Harusi Ya Fidel Odinga
Mwana wa kiume wa Waziri Mkuu Raila Odinga Fidel Castro Odinga hii leo kwa mara ya pili amefunga pingu za maisha na aliyekuwa mchumba wake kutoka Eritrea Lwam Getachew Bekele katika kanisa la Othordox hapa jijini Nairobi. Sherehe hiyo fupi ya harusi ilihudhuriwa na familia za familia hizo mbili na wageni wachache waalikwa akiwemo balozi wa Eritrea humu nchini Beyene Russom.
















